Shilingi ya Tanzania itaendelea kuporomoka kila mara endapo nchi itaendelea kutegemea bidhaa toka nje kwa kiwango kikubwa kuliko inavyozalisha ndani.
Akizungumza
na MPEKUZI Profesa Prosper Ngowi toka Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema
watanzania wasitegemee miujiza wa kukua kwa uchumi wa nchi yao endapo
nchi itaendelea kuwa dampo la bidhaa toka nje ya nchi.
Alisema
Tatizo kubwa la Tanzania ya leo ni kukubali kwake kutumiwa kama dampo
la bidhaa nyingi toka mataifa ya nje, tena nyingi ya bidhaa hizo zikiwa
feki zisizio kuwa na viwango.
Alisema hali imezidi kuwa mbaya katika miaka ya hivi karibuni baada ya Tanzania kuridhia masuala ya soko huria.
“Hebu
angalia hata baadhi ya huduma za kijamii hapa nyumbani leo zinapatikana
kwa kutumia dola suala linalochangia kuiporomosha thamani ya shilingi
yetu” alisema Profesa Ngowi.
Alisema
njia pekee inayoweza kuiokoa shilingi ya Tanzania ni nchi kuanza
kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa za ndani ili mwisho wa siku tuweze
kuuza nje kwa wingi.
“Haiwezekani
ukakubali kugeuka dampo la bidhaa nyingi tena mbovu toka nje halafu
utarajie dhamani ya fedha yako ikawa juu hiyo haiwezekani” alisema
Profesa Ngowi.
Alisema
hata mamlaka husika nazo kwa kiwango kikubwa zimekuwa zikichangia kwa
kiwango fulani kuporomoka kwa dhamani ya shilingi yetu kwa kuruhusu
bidhaa kuingia nchini kiholela.
Alisema
nilazima tuwe makini na baadhi ya sera tunazoletewa na wenzetu toka nje
kwani mara nyingi huwa zinalenga kutumaliza ili tuendele kuwa tegemezi
toka kwao.
Alisema
wakati Tanzania inapata uhuru wake viongozi walihimiza sana nchi
kuzalisha ndani kwa maana ya kuiwezesha nchi kupata fedha za kigeni kwa
wingi.
“Hali
hii ilikuja kubadilika mara baada ya kuletewa mashariti ya kiuchumi
nasi tukayapokea bila hata ya kujiuliza madhara yake ya baadae” alisema
Profesa Ngowi.
Alisema
kama nchi inatakiwa tuache kufikiria ndoto za alinacha kuwa uchumi wa
nchi unaweza kukua kwa kwa nchi kuendelea kuwa dampo la bidhaa toka nje
ya nchi.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.