Jumuiya na Taasisi za Kiisalam nchini, imetoa tamko na kuipa serikali siku 15 kabla ya kufanya maandamano nchi nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakidai kufunguliwa kwa madrasa zilizofungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi.
Masharti
mengine ni kuachiliwa huru au kwa dhamana masheikh na maimamu
waliokamatwa wakituhumiwa kutoa mafunzo na mazoezi ya kigaidi.
Maeneo
ambayo madrasa hizo zaidi ya 10 zimefungwa ni katika mikoa ya
Kilimajaro, Dodoma na Mtwara. Tamko hilo pia lilisema jeshi hilo
linawatuhumu kwa kukusanya watoto na kuwafundisha elimu ya dini katika
mazingira yasiyofaa na kuwapo kwa taarifa za watu wenye milipuko
misikitini na kujihusisha na ugaidi.
Mwenyekiti
wa jumuiya hiyo, Sheikh Musa Kundecha, alisema jeshi hilo limekuwa
likiwakamata watu hao usiku na kuwapeleka katika vituo vya polisi, na
kuwahoji.
Alisema
jeshi hilo limekuwa likifanya kazi za maofisa wa ustawi wa jamii na
elimu, kufanya ukaguzi katika maeneo ambayo watoto hao wanafundushwa
elimu ya dini ya kiislamu.
“Mkakati
wa operesheni hii unakiuka utu, haki za binadamu, kikatiba na ni
uchochezi dhidi ya Waislamu kuwafanya wachukiwe na jamii, tunawatunza
yatima katika maeneo jirani na madrasa na kuwapa elimu ya kidini siyo
kosa, tunatimiza wajibu wa kidini. Wajibu wa serikali ni kutulinda,
lakini tunawekwa katika mazingira ya hatari,” alisema Kundecha.
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, alisema
ulifanikiwa utafiti, kabla ya jeshi hilo kuchukua hatua za kufunga
baadhi ya madrasa na kuwakamata watu hao.
“Katika
maeneo ya mikoa hiyo ni kweli kuna suala hilo, na watoto ambao wana
umri wa kuwa shule walikutwa pale, hivyo tukataka kufahamu na yajulikane
mafunzo wanayopewa,” alisema Nantanga.
Alisema
kuendelea kushikiliwa kwa baadhi ya watu waliokamatwa na kunyimwa
dhamana kunatokana na jeshi hilo kutojiridhisha au kutokamilika kwa
taratibu za dhamana.
“Pale
mtuhumiwa atakapoachiwa, ni lazima polisi wajiridhishe kabla ya
kumpatia dhamana mtuhumiwa. Hadi hivi sasa, kama wizara hatujapokea
tamko lolote kuhusu jambo hili, tunasubiri kupokea rasmi tamko, na
tutaliweka mezani na kulifanyia kazi,” aliongeza.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.