Mchaka Zaidi

Wednesday, April 15, 2015

Lipumba: Siku Ya Uchaguzi Mkuu Itatangazwa Na NEC Na Si Vinginevyo



 
Mwenyekiti wa taifa wa Chama  cha Wananchi (CUF),Profesa   Ibrahim Lipumba akizungumza na baraza la uongozi wa chama hicho (hawapo pichani) iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Nassor Ahmed na kushoto ni makamu Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Taifa,Duni Haji.

 
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,akisikiliza kwa makini katika ufunguzi wa mkutano Baraza la uongozi wa chama wananchi  (CUF) na kulia ni Naibu Katibu        Mkuu Zanzibar Nassor Ahmed iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Baraza la Uongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba  (hayupo pichani) iliyofanyika  jana Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo)

Na  Avila Kakingo.
TUME ya Taifa ya  uchaguzi (NEC) ndiyo inayotakiwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu mwaka huu pamoja na kutangaza matokeo ya viongozi watakao kuwa wameshinda katika uchaguzi huo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama  cha Wananchi (CUF),Profesa  Ibrahim Lipumba wakati akifungua mkutano Baraza la uongozi wa chama hicho  jana jijini Dar es salaam.  
 
Lipumba alisema kuwa  ucheleweshwaji wa  uandikishaji wa daftari la wapiga kura  linatia shaka kutokana na kutokukamilika kwa zoezi hilo mpaka sasa.

Aidha alisema kuna  vifungu vya sheria kwenye katiba pendekezwa virekebishwe hasa kifungu cha Tume ya Taifa  Uchaguzi (NEC) kutangaza Matokeo ya uchaguzi mkuu  ya Rais atayekuwa ameshinda na  awe amepata kura zaidi ya asilimia 50 pia matokeo hayo yahojiwe au  yakikishwe na mahakama.
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.