Mchaka Zaidi

Wednesday, April 22, 2015

Mapambano Bado Yanaendelea......Jana CHADEMA na ACT-Wazalendo Nusura Wakutane Uso Kwa Uso Nyumbani Kwa Baba wa Taifa. Vurugu Za Mnyika Ziligonga Mwamba Kwa Mara Nyingine


Mtoto wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Andrew Nyere, akiteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na kuvaa kofia ya Chama cha ACT-Wazalendo wakati viongozi wa chama hicho walipofanya ziara kijijini Mwitongo Wilayani Butiama.
Viongozi  wa Chama cha ACT-Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), jana nusura wakutane uso kwa uso nyumbani kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, walipokwenda kuzuru kaburi lake kwenyeKijiji cha Mwitongo, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.
 
Msafara wa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Bw. John Mnyika, ndio ulioanza kuwasili kijijini hapo na baada ya kuzuru kaburi, waliondoka ukawasili msafara wa ACT ukiongozwa na Kiongozi wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe.
 
Msafara wa ACT, ulifika kijijini hapo baada ya chama hicho kumaliza ziara ya kukitangaza, kukitambulisha chama na viongozi wake kwenye mikoa mbalimbali nchini.
 
Akizungumza mara baada ya kuwapokea viongozi wa ACT,Mzee wa Ukoo wa Burito ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wazee wa Butiama, Jack Nyamwaga, alisema muda mfupi uliopita walikuwepo viongozi wa CHADEMA.
 
"Baada ya viongozi hao kufika hapa Mwitongo, walisema kuna viongozi wanakuja lakini tusiwape ushirikiano wakidai kama ni suala la kupinga ufisadi, CHADEMA wamelipigia kelele ili kumuenzi Mwalimu Nyerere.
 
"Kimsingi kila mtu anaruhusiwa kufika hapa Mwitongo katika kaburi la Mwalimu na sisi kama wanafamilia, tunampokea kila mtu lakini si kazi yetu kusema nani aje, nani asije," alisema.
 
Aliongeza kuwa, viongozi wengi wamekuwa wakimuenzi Mwalimu Nyerere kwa maneno si kwa vitendo..."ACT mmeanza vizuri na mtamaliza vizuri, nawatakia kila la heri kama kweli mtamuenzi Mwalimu kwa vitendo," alisema Mzee Nyamwaga.
 
Kwa upande wake, Bw. Kabwe alisema wao watamuenzi Mwalimu kwa vitendo ndio maana wameweka msingi huo katika ilani ya chama chao.
Mtoto wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Andrew Nyerere, akimkabidhi kofia ya CCM, Kiongozi wa Chama cha  ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na kuvaa kofia ya Chama cha ACT-Wazalendo wakati viongozi wa chama hicho walipofanya ziara kijijini Mwitongo Wilayani Butiama.
**
Alisema lengo la kumalizia ziara hiyo kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere ni kutokana na kuuenzi mchango wake kwa Taifa na Watanzania ndio maana walianzia ziara yao mkoani Ruvuma.
 
"Tumefika hapa na viongozi wenzangu wa ACT kwa sababu ya kutambua mchango wa Mwalimu kwa Taifa...chama chetu kitayaenzi mambo yote ambayo Mwalimu alikuwa akiyakataa kwa vitendo na Katiba yetu inatamka hivyo," alisema Bw. Kabwe.
Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.