Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Hassan Suluhu amesema kero mbalimbali za Muungano zilizoibuliwa zimeanza kufanyiwa tathmini na Serikali.
Suluhu
alisema hayo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
wakati alipokuwa akizindua onesho la miaka 51 ya muungano wa Tanganyika
na Zanzibar.
Alisema
moja ya hatua zilizoanza kuchukuliwa na Serikali juu ya kero hizo ni
kuyaingia baadhi ya masuala ya Muuungano katika Katiba Inayopendekezwa
kwa lengo la kuyatambua.
“Kutokana
na kuibuka kwa kero hizo, Serikali ilikaa na kufanya tathmini na ndiyo
maana hata katika Katiba Inayopendekezwa yametajwa na ndiyo maana
tunasema ipigiwe kura ya ‘ndio’,” alisema.
Suluhu
alisema anawashangaa watu wanaoupinga Muungano kwa madai kuwa huenda
wana sababu zao kwani watanzania wengi bado wanaupenda na kuunga mkono.
Alitoa
wito kwa watanzania kufika katika makumbusho hayo yaliyopo Posta jijini
humo kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali juu ya Muungano huo ili
wayajue na kuyaelewa.
“Njooni
mjifunze mambo ya msingi juu ya Muungano wetu, wenzetu wa makumbusho
wametenga siku saba kwa ajili yenu, mje mjifunze ili muuelewe vizuri
muungano huu,” alitoa wito.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.