Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya
wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo
mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa
tumbo hilo limeyeyuka.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga
vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano
wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.
Mwandishi alizungumza na
baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki
chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.
“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’
kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,”
alisema mmoja wa wanachuo hao.
Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi
wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila
majibu.
Baadaye alitumiwa ujumbe wa kuulizwa kuhusu sakata hilo ambapo alijibu: “Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.”
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.
Chanzo: Gpl/Gazeti la Amani, Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.