Mchaka Zaidi

Monday, June 22, 2015

Ni kweli Rose Muhando kachukua pesa na hajaenda kwenye show?! #U Heaard!!

rose-muhanda
Leo kwenye @UHeard na Soudy Brown ilikua inamuhusu msanii mkubwa wa injiliTanzania, Rose Muhando. Baada ya mipango ya show na promota kwenda chaka, promoto akaamua kumuendea Soudy Brown hewani na kumuelezea kisa chote.

Rose Muhando aliingia mkataba wa millioni tatu na laki tano kwa ajili ya kufanya showNjombe mkoani Iringa, baada ya makubaliano kukamilika ikabakia Rose Muhandokwenda kutumbwiza kwenye Tamasha hilo la kiinjili huko Njombe, lakini siku ya siku Roseakaingia mitini, akipigiwa simu anasema yupo njiani na dakika ya mwisho akaamua kuzima simu. Na kwenye tamasha hakuonekana kabisa!
Kwa upande wa waandaji, wanasema hasara walioingia ni zaidi ya millioni sita, watu walioingia nae mkataba wamesema kwamba hakuna cha msamaha wakiupendo kwani kitu kama hichi alishawahi kukifanya huko Mbeya amabako mpaka sasa wanamtafuta msanii huyo wa injili ili wamueke ndani, watu wa Njombe wamesema kua wanataka pesa yao irudishwe na kama haitowezekana basi hatua za kisheria zifuate juu yake.
Stori nzima ipo kwenye hii sauti hapa chini mtu wangu.
BOFYA HAPA KUSIKILIZA!!!!!

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.