Mchaka Zaidi

Monday, June 22, 2015

Album ya Amini na mkewe ipo? Hussein Machozi kaacha muziki?? Diamond kazuia collabo za nje? Ziko zote hapa (Audio)

Studio


Tunahesabu mwaka wa pili sasa hivi tangu staa wa Muziki ambae ni moja ya matunda mazuri ya THT, Amini Mwinyimkuu aingie kwenye Headlines baada ya kufunga ndoa.. aliyefunga nae ndoa ni msanii mwenzake pia, walituahidi album ya pamoja.. vipi huo mpango unaendaje mpaka sasa?
2
Amini na Farida siku ya ndoa yao mwaka 2014
Amini ana majibu kwenye #255, amesema mpango uko palepale hakuna kitu kimebadilika na tayari kuna nyimbo zimerekodiwa na nyingine zinaendelea kupikwa.. time yoyote album ikikamilika basi tutaanza kuenjoy muziki mzuri wa Wanandoa hao!
Hussein Machozi ndio kusema anauacha huu muziki? Jamaa amesema zamani alikuwa anacheza sana mpira wa miguu, baadae akaingia kwenye muziki lakini wamerudi kwenye meza ya mazungumzo na timu ya Mtibwa Sugar na time yoyote atarudi uwanjani kwenye soka.
.
Hussein Machozi yuko zoezini na watu wake.
Hussein kasema yeye na muziki bado ni damdam, utamwona kwenye soka na kwenye muziki bado yupo pia !!
Diamond Platnumz nae kuna kingine kutoka kwake leo, jamaa kasema ameamua kusimamisha kufanya collabo na wasanii wa nje kwa kuwa mara ya kwanza alizipiga nyingi ili kutafuta upenyo mzuri Afrika ijue muziki mzuri wa TZ.. YES, kapiga kazi nyingi na mastaa wengi na hiyo imeuweka muziki wa TZ mahali pazuri, kwa sasa collabo hizo zitasimama.
Diamond
Diamond amesema collabo ya mwisho kufanya kwa sasa itakuwa ya yeye na KCee, staa kutoka Nigeria.
Diamond anasema japo kaamua hivyo lakini kuna foleni ya mastaa ambao nao wameomba nae collabo mpaka sasa wengine hata hawakumbuki majina yao !!
BOFYA 255 iko hapa mtu wangu, utamsikia Diamond Platnumz, Amini na Hussein Machozi..

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.