Mchaka Zaidi

Thursday, June 18, 2015

Mtuhumiwa wa Ukatili Aachiwa Huru Mahakamani


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemwachia huru mtuhumiwa wa kesi ya ukatili dhidi ya mtoto, Georgina Makasi.
 
Hatua ya kuachiwa huru kwa mtuhumiwa huyo, imekuja baada ya mashahidi upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka.
 
Mahakama ilimwachia huru mtuhumiwa huyo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassani kwa kuongozwa na wakili wa Serikali, Felista Mosha.
 
Awali shtaka hilo lilikuja kwa ajili ya hukumu, lakini mahakama ililazimika kumwachia huru mshtakiwa kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha ushahidi wao mahakamani.
 
Juni 6, mwaka 2012, mtuhumiwa Georgina anadaiwa alimpiga mtoto Halima Seif kwa kutumia pasi ya moto, kinyume cha sheria na haki za mtoto.
Chanzo: Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.