Mwaka 2009 Kenya waliingia kwenye Headlines kuhusu ishu ya Ikulu ya nchi hiyo kununua magari ya kifahari na ikawa skendo kubwa sana kwa vile wakati magari yananunuliwa RaisMwai Kibaki alikuwa likizo wakati huo… Bunge la Tanzania imesikika pia ishu ya kulalamikiwa kuhusu Serikali kutumia magari ya kifahari, stori iko tofauti sana toka Ugiriki.
Yanis Varoufakis ni Waziri wa Fedha wa Ugiriki, jamaa hata hana mambo mengi yani.. haitaji kuzinguana kwenye foleni barabarani wala nini, usafiri wake kwenda Ofisini ni pikipiki aka bodaboda !!
Kiutaratibu kabisa Kiongozi wa nafasi yake anatakiwa awe kwenye gari na awe na dereva wa kumwendesha, lakini huu ndio usafiri wa chaguo la moyo wake kabisa mtu wangu !!
Unafikiri Bongo tutaweza!!!!
Chanzo: millardayo.com
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.