Waziri
mkuu wa zamani Mh.Edward Lowasa aliyeko kanda ya ziwa kutafuta
wadhamini amepata wakati mgumu alipowasili mkoani Mara baada ya makundi
ya wananchi wakiwemo vijana,wanawake na watoto kumfuata kila
alikokwenda wakitaka wapewe nafasi ya kumueleza kero zao jambo
lililosababisha zoezi la kumdhamini kuwa gumu licha ya kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa.
Heka
heka za wananchi kutaka kuzuia msafara wa Mh.Lowasa zilianza mapema
asubuhi wakati anawasili kwenye uwanja wa ndege wa musoma ambapo vijana
walizuia msafara wake kutoka kwenye uwanja huo wakitaka wapewe nafasi
ya kuonana naye.
Baada
ya waratibu wa msafara huo kufanya kazi ya ziada ya kufanikiwa kutatua
changamoto hiyo Mh.Lowasa aliekea katika wilaya ya Bunda na licha ya
kusimamishwa na wananchi njiani hali ilikuwa ngumu zaidi katika ofisi
ya CCM wilaya ya hiyo kutokana na watu kujitokeza kwa wingi.
Hata
hivyo pamoja na maelfu ya wananchi hao wanaounga mkono safari ya
matumaiani kuwa na shauku ya kumueleza Mh.Lowasa shida zao alishindwa
kuwasikiliza kutokana na kubanwa na kanuni na aliwaomba kuwa watulivu
na kuendelea kuiombea kheri safari ya matumaini.
Mh.Lowasa
akiwa katika mkoa wa Mara amepata idadi kubwa ya wadhaamini pia
amefika nyumbani kwa hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere na kupewa
baraka, kisha kuweka shada la maua kwenye kaburi na pia ametembelea
wilaya ya Tarime na Musoma.
Mh.Lowassa
ambaye ameshatembelea mikoa ya Mwanza Geita,Zanzibar na Pemba
anaendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mkoa wa Simiyu.
Maelfu ya Wananchi wakiwa wameuzuia Msafara wa Lowassa wakishinikiza kumuona, hali iliyowalazimu Polisi na waratibu wa msafara ya kutumia njia mbadala kutatua changamoto hiyo
Maelfu ya Wananchi wakiwa wameuzuia Msafara wa Lowassa wakishinikiza kumuona, hali iliyowalazimu Polisi na waratibu wa msafara ya kutumia njia mbadala kutatua changamoto hiyo
Mh. Lowassa alipotembelea Kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwl. J.K. Nyerere
Chanzo: mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.