Mchaka Zaidi

Thursday, June 25, 2015

Kocha Mkuu Mpya na mabadiliko,soma HAPA

.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa leo(jana) ameushukuru uongozi wa shirikisho la soka nchini TFF kwa kumteua kushika nafasi ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa kwa kusaidiana na kocha kutoka visiwani Zanzibar Hemed Morocco.

Mkwasa amesema wadhifa aliopewa na TFF, una hadhi kubwa kwake pamoja na kwa taifa zima la Tanzania, hivyo amewaomba mashabiki wa soka nchini kuwa na uvumilivu pamoja na kumuonyesha ushirikiano katika kazi yake hususan katika kipindi kigumu ambapo Taifa Stars inakabiliwa na mchezo wa mkondo wa pili wa kuwani kufuzu kucheza fainali za mataifa bingwa barani Afrika CHAN dhidi ya Uganda ambao wapo mbele kwa mabao matatu kwa sifuri.
Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.
Ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho(leo) alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo June 24(jana) alisema ‘Baada ya kutangaza kikosi cha wachezaji ambacho kitakuwa na kazi ya kubadili matokeo ya kufungwa mabao matatu kwa sifuri na kusaka ushindi wa zaidi ya mabao manne kwa sifuri ugenini huko jijini Kampala mnamo July 04′
Picha kwa hisani ya Father Kidevu
WALIOACHWA: Kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’ , wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba kwa mujibu wa salehjembe.blogspot.com
Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting.
Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.
KIKOSI KAMILI:
Mwadini Ally-Azam
Ally Mustapha-Yanga
Mudathir Khamis-KMKM
Shomari Kapombe-Azam
Michael Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed Hussein-Simba
Mwinyi Hajj-KMKM
Nadir Haroub-Yanga
Kelvin Yondani-Yanga
Aggrey Morris-Azam
Hassan Isihaka-Simba
Jonas Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon Msuva-Yanga
Said Ndemla-Simba
Ramadhan Singano-Simba
Salum Telela-Yanga
Frank Domayo-Azam
Atupele Green-Kagera Sugar
Rashid Mandawa-Mwadui
Ame Ally-Azam
Deus Kaseke-Yanga
Chanzo: Millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.