Wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayobadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo iliyopewa jina la S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono huku ikiwa na uwezo wa kubadili rangi tofauti kulingana na bakteria waliopo.
Miongoni mwa wafumbuzi waliofanya uvumbuzi huu ni Daanyaal Ali (14), Muaz Nawaz (13) na Chirag Shah (14), ambapo kufuatia ufumbuzi huo tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ”the TeenTech” sambamba na kutunukiwa pauni elfu moja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.
Akifafanua juu ya uvumbuzi huo, mmoja wa wanafunzi hao Daanyaal Ali amesema kuwa “Tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini kwa ajili ya kizazi kijacho”.
Aliongeza kuwa “Swala la usalama wa mpenzi ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaumbele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia”
Kwa upande wake Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Maggie Philbin alisema kuwa ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa lengo la kuboresha maisha ya mwanadamu.
Chanzo: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.