JESHI la Polisi limefanikiwa kukamata Silaha, watuhumiwa wa uhalifu wa kutukia silaha katika oparesheni iliyoendeshwa kwa nyakati tofauti katika Jiji la Dar es Salaam.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Jiji la Dar es Salaam(DCP), Simon Sirro
alisema baadhi ya silaha hizo ni pamoja na bunduki aina ya SMG na jumla
risasi 59.
Sirro
alisema kuwa tarehe Juni 3 mwaka huu mtuhumiwa Hemed Mrisho
anayejulikana kwa jina la Buda (31) mfanyabiashara, mkazi wa Tabata
Kinyelezi alikutwa na bunduki hiyo iliyofutwa namba zake ikiwa na jumla
ya risasi 10.
“Mtuhumiwa
alikamatwa kutokana na taarifa kutoka kwa msiri kuwa anajihusisha na
uhalifu wa kutumia silaha na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa
mtuhumiwa alikuwa akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa” alisema Sirro.
Alisema
katika tukio lingine Jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata bastola moja
na maganda ya risasi aina ya SMG maeneo ya Kiwalani Minazi mirefu
wilaya ya Ilala.
Alisema
kuwa bastola hiyo yenye namba 05532 ilikutwa eneo la tukio baada ya
majambazi kuitelekeza mara baada ya kuzingirwa na wananchi waliotaka
kuwakamata.
“Majambazi
hao walikuwa wamefanya tukio la uporaji maeneo ya Vingunguti wakitumia
pikipiki aina ya boxer na katika tukio hilo walimpiga mtoa taarifa na
kitako cha bunduki waliyokuwa nayo na kumpora pikipiki na pesa taslim
shilingi 300,000 lakini hata hivyo walifanikiwa kutoroka” alisema Sirro.
Aliongeza
kuwa katika operesheni iliyoendeshwa Mei 25 mwaka huu na idara ya
Interpol jijini Dar es Salaam ya kukamata magari, madawa ya kulevya na
uhalifu mwingine walifanikiwa kukamata vipande 20 vya pembe za ndovu.
Sirro
alisema katika tukio hilo maeneo ya Kimara Suka katika ukaguzi huo
alishuka kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 39 na 45 kwa dhumuni la
kukodi pikipiki na alipowaona askari alitupa kifurushi na kukimbia.
Katika
tukio lingine jeshi la polisi walifanikiwa kukamata kontena lenye namba
00LU2876031 likiwa na rola 15 za nyaya za umeme mali ya Tanesco pamoja
na watuhumiwa saba.
Sirro
alisema kuwa nyaya hizo zinathamani ya shilingi milioni 150 zilizoibiwa
Februari 26 mwaka huu zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani Kagera kwa
ajili ya mradi wa umeme vijijini (REA).
“Tulipata
taarifa kwa msiri kuwa kuna kontena limefichwa katika kiwanda cha
kutengenezea matofali na Polisi walipofika walimpata mmiliki
aliyetambulika kwa jina la Donesia Aidan (40) ambaye ni mtuhumiwa wa
sita na walipopekua kontena hilo walikuta rola za nyaya zipatazo 15” alisema Sirro.
Chanzo: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.