Waziri
wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri ambaye pia ni miongoni mwa wagombea
waliochukua fomu za kuwania mbio za uraisi wa awamu ya tano amesema
hawezi kuthubutu kuzungumza chochote mbele ya hadhara ya wananchi katika
kipindi hiki kigumu cha kutafuta wadhamini na kwamba kufanya hivyo
nikukiuka maadili ya chama chake.
Akizungumza
mjini Bukoba wakati wa akitoa shukrani zake kwa waliojitokeza
kumdhamini, waziri Magifuli amewaambia wadhamini wake mkoani Kagera
kwamba hawezi kuongea kitu chochote juu ya nini atawafanyia wananchi
endapo atachaguliwa kushika nafasi ya urais wa awamu ya tano na kuongeza
kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujafika kwa kuwa kampeni hazijaanza,
hivyo wanaotoa ahadi wanakiuka kanuni za chama.
Chanzo: mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.