Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba pamoja na Mke wake katika ukumbi wa makao makuu ya CCM Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa NEC Dodoma.
Mke wa Mwigulu Nchemba akiwasalimia Waandishi wa Habari.
Naibu waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika mkutano na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais leo.
Naibu
Waziri waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba leo amechukua fomu ya kugombea
urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa atateuliwa na chama
chake cha Mapinduzi kupeperusha bendera ya Tanzania katika uchagauzi
mkuu ujao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari amesema kwamba atahakikisha anaboresha uchumi
kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuboresha njia kuu za wananchi kupata
kipato. Kufufua viwanda vilivyokufa ili kutoa ajira kwa vijana pamoja
na kudhibiti madawa ya Kulevya, Rushwa na ufisadi.
Amesisitiza kuwa Rais Kikwete ndiye rais wa mwisho kutawala Tanzania maskini.
Chanzo: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.