Tume ya uchaguzi nchini (NEC)imesema tarehe ya Uchaguzi mkuu Mwaka huu iko pale pale ambapo ni siku ya terehe 25 mwezi octoba mwaka huu.
Kauli ya NEC inakuja ikiwa ni siku moja kupita
baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe
kuitangazi serikali kiama endapo itasogeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu
Akifanunua
Kauli hiyo ya Mbowe leo Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa NEC
Jaji mstaafu Damian Lubuva wakati wa Mkutano na Waandishi wa
Habari amesema taarifa zinazosemwa na wanasiasa kwamba tume hiyo
itasogeza mbele uchaguzi Mkuu si za
kweli na zinalengo la kuwachanganya wananchi kwani tume hiyo inakwenda
vizuri na
uandikishaji wa Mfumo mpya wa BVR.
Jaji Damian ameongeza kuwa kwa sasa
Uandikishaji wa Wapiga kura kwenye Mkoa wa mdogo wa Njombe unatarajia kumalizika
kesho na kuanza rasmi uandikishaji kwenye mikoa mingine ya Mtwara,Lindi na
Iringa ambapo amasema kwa sasa watafanya kwa kasi zaidi.
Amebainisha kuwa tatizo lililokuwa
linawakabili kwa kuwa na mashine chache za uandikishaji wamelitatua
kwakuwa sahivi tayari mashine nyingine 1600 zinatarajiwa kuwasili kesho, jambo ambalo anadai litafanikishwa
kasi ya uandikishaji.
Aidha,amesema shehena nyingine ya
mashine inatarajiwa kuja tarehe 25 mwezi huu na mpaka ifikapo mwezi wa Sita mwaka
huu watakuwa wameshapata mashine zote elfu nane walizokuwa wakizihitaji , jambo
ambalo amesema litawafanya wamalize kuwaandisha wananchi nchi nzima
mwezi wa saba mwaka huu.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.