Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Hellen Riwa, alisema
mahakama imemwachia huru mshtakiwa huyo kutokana na upande wa mashtaka
kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa huyo.
Alisema
katika ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haioneshi wazi kwamba
mbunge huyo aliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha.
Alisema
kwa hadhi aliyokuwa nayo mbunge hawezi kuchukua wala kuomba rushwa sh.
milioni moja na kuhoji kama mbunge anafanya hivyo na watu wa chini
wafanyaje.
Mbali
na kumwachia huru mshtakiwa huyo pia, hakimu alimuonya mshtakiwa huyo
awapo jimboni kwake kujihadhari na kuepuka kushika vitu vya watu ili
aweze kujilinda na vitu kama hivyo.
"Kama
una tofauti na watu katika jimbo lako kuwa makini na ujihadhari pamoja
na kujirekebisha kama una tabia ya kuombaomba jirekebishe na kuepuka
kugusa vitu vya watu," alisema hakimu.
Alisema mahakama hiyo haikutia shaka pale mshtakiwa alipojitetea mwenyewe na kukana kufanya makosa hayo.
"Kutokana
na ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuithibitishia mahakama
pasipo shaka kwamba mbunge huyo ametenda makosa hayo, mshtakiwa upo
huru kuanzia sasa," alisema.
Badwel
alikuwa akabiliwa na shitaka la rushwa ambapo anadaiwa kutenda kosa
hilo kati ya Mei 30 na Juni 2, 2012, katika maeneo tofauti mkoani Dar es
Salaam ambapo alishawishi apewe rushwa ya shilingi milioni 1 kutoka kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Sipora Liana.
Kesi hiyo ambayo imedumu kwa takriban miaka mitatu sasa ilifikia tamati jana kwa mbunge huyo kuachiwa huru.
Awali
wakati kesi hiyo ikiendelea kunguruma mahakamani hapo mshtakiwa huyo
katika utetezi wake alidai hajawahi kuomba wala kupokea rushwa ya sh.
milioni 1 kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga Sipora Liana wala kuwa na nia kama hiyo.
Wakati
huo huo, Mahakama hiyo imeahirisha kesi ya mauaji inayowakabili
washtakiwa 11 wanaokabiliwa na shtaka la kumuua kwa kukusudia
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi
kutokana na upepelezi kutokamilika.
Mbele
ya Hakimu, Thomas Simba, wakili wa Serikali Honolina Munisi, aliiomba
mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa upelelezi haujakamilika.
Hata hivyo, Hakimu Simba, aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 12, mwaka huu.
Washtakiwa
hao ni Chibago Magozi (32), Juma Kangungu (29), Msungwa Matonya (30) na
Mianda Mlewa (40) wote wakazi wa Vingunguti, Dar es Salaam na John
Mayunga (56) mkazi wa Kiwalani.
Wengine
ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dkt. Mvungi, Longishu Losingo (29),
dereva na mkazi wa Kitunda, Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata
Darajani, Paulo Mdonondo (30), mkazi wa Buguruni, Zacharia Msese (33) na
mkazi wa Mwananyamala, Ahmad Kitabu (30).
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.