Mchaka Zaidi

Saturday, April 25, 2015

Afande Sele: Nikichaguliwa Kuwa Mbunge Nitakataa Posho na Mishahara Mikubwa


Mwana hip hop na Bongo Fleva nchini, Afande Sele, ameweka wazi kwamba hata kama atakuwa mwakilishi wa wananchi katika bunge la mwakani, hataweza kuacha kufanya muziki kwa kuwa ndiyo njia ya kumuingizia kipato.
 
Alisema licha ya kuwa bungeni, atakuwa akitegemea zaidi fedha zinazotokana na muziki wake badala ya kufikiria mishahara minono na posho zinazopatikana bungeni.
 
“Kazi yangu ya muziki siwezi kuiacha, ndiyo itakayoniongoza katika maisha yangu, kwa kuwa nitakapokuwa bungeni licha ya kuwa na utetezi mwingine kwa wananchi, lakini pia nitapinga na kukataa posho na mishahara minono wanayopata wabunge kiasi kwamba wanasahau walipotokea,’’ alieleza Afande
 
Afande, ambaye sasa ni mwanachama wa chama Kipya ya ACT, aliongeza kwamba ili wasanii waweze kuwatumikia vema wananchi, baada ya kuwa wabunge lazima wakatae posho na mishahara minono.
 
“Wasanii wengi waliopo bungeni wanajisahau kwa kuwa wanapopata posho na mishahara minono wanasahau walipotoka na kujitofautisha na wananchi na ukishachukua fedha hizo huwezi kuwatetea wananchi, lakini mimi nikienda huko nitapiga vita dhidi ya posho na mishahara hiyo minono ili fedha hizo zielekezwe kwenye shughuli nyingine za maendeleo,’’ alieleza.
 
Aliongeza kwamba hatajali hata akilipwa kiasi kidogo cha mshahara kwa kuwa lengo lake la utetezi litakuwa limekamilika na wananchi wengi Tanzania watanufaika nalo kama posho na mishahara minono itapunguzwa ama kufutwa kabisa.
Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.