Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote
Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.
Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
Wakati taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao
ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la
kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo
maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo
walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa
imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya
waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita.
Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na
viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri
kiongozi huyo afike kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano
zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu
ambapo alisomewa mashitaka mawili ya kutoa lugha ya matusi na kushindwa
kutunza silaha.
Askofu huyo ameachiwa kwa dhamana na kesi yake itaendelea Mei 4 mwaka huu.
Askofu huyo ameachiwa kwa dhamana na kesi yake itaendelea Mei 4 mwaka huu.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.