Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, ameitaka Serikali kuhakikisha madereva wote wa magari ya mizigo na mabasi ya abiria, wanapewa mikataba ya ajira kabla ya Aprili 17, mwaka huu.
Bw.
Kabwe aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Viwanja vya Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege, mkoani Morogoro baada ya
kushiriki mazishi ya watu zaidi ya 17 walioteketea kwa moto kwenye ajali
ya basi la abiria la Nganga na Mitsubishi Fuso.
Ajali hiyo ilitokea kwenye eneo la Iyovi, Kijiji cha Msimba, Tarafa ya Mikumi, mkoani humo.
Mazishi
hayo yalifanyika katika makaburi ya Msamvu, Kata ya Ruaha, wilayani
Kilosa yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, taasisi
na wananchi.
Alisema
vifo hivyo vinatia uchungu kutokana na marehemu hao kuzikwa katika
kaburi moja na kufafanua kuwa, amefanya mazungumzo na viongozi wa
madereva wa mabasi ya abiria na kudai kama ikifika Aprili 17, mwaka huu
hawajapewa mikataba ya ajira, watagoma Aprili 18, mwaka huu,
"ACT-Wazalendo tunaitaka Serikali iwabane wamiliki wa mabasi ili hawa madereva wapewe mikataba," alisema.
Akiuzungumzia
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Bw. Kabwe alisema wao hawaupingi
umoja huo kwani kazi wanayoifanya ni kuiondoa Serikali ya CCM madarakani
lakini hawahitaji vyama visivyo na uzalendo.
"Asilimia
50 ya viwanda vya sukari viko hapa Morogoro na hakuna kiwanda vipya
zaidi ya vile alivyojenga hayati Mwalimu Nyerere; lakini vinawanyonya
wakulima wa miwa na kusababisha kilimo chao kutowafaidisha," alisema.
Alisema
mkoa huo ni wa sita kuchangia pato la Taifa upande wa Tanzania Bara,
lakini upo chini kwa maendeleo ya watu ukishika nafasi ya 11.
Aliongeza kuwa, changamoto kubwa ipo kwenye elimu ambapo kati ya watu 100 mkoani humo, wanane ndio wenye elimu ya sekondari.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bi.Anna Mghwira, alisema
ACT itaondoa migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha kuna mipaka ya wakulima,
wafugaji.
Alisema watapiga marufuku wawekezaji kuwakodishia ardhi wakulima ili ardhi hiyo imilikishwe kwa wakulima.
"Kumuenzi Mwalimu ni kukataa ubinafsishaji holela na ujamaa ulijenga viwanda...mfumo wa sasa umeuza viwanda
na watu hawana ajira," alisema Bi. Mghwira.
Aliongeza
kuwa, ujamaa ulikuwa na faida zaidi kuliko sasa; hivyo chama hicho
kitamuenzi Mwalimu kwa kupinga sera za ubinafsishaji na watahakikisha
mali za wananchi hazitaifishwi bali watarekebisha makosa ya
ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za Taifa zilizouzwa.
Wakati
huo huo habari kutoka Singida zinaarifu kuwa, Bw. Kabwe na viongozi
wengine wa chama hicho, kesho wanatarajia kuanza ziara ya siku mbili
mkoani humo ili kuimarisha chama.
Mwenyekiti
wa chama hicho mkoani humo, Bw. Wilfred Kitundu, alisema Bw. Kabwe
atafungua matawi tisa na ofisi tatu za kanda, kuhutubia mkutano wa
hadhara Mjini Singida.
"Ziara
hii itaanzia katika Wilaya ya Manyoni kuanzia asubuhi ambako atafungua
Tawi la Kitinku, pia atakwenda Mjini Singida ambako atafungua matawi
matatu ya Kisaki, Utemini, Ukombozi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.