
Jumuiya na Taasisi za Kiisalam nchini, imetoa tamko na kuipa serikali siku 15 kabla ya kufanya maandamano nchi nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakidai kufunguliwa kwa madrasa zilizofungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi.
Mtoto wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Andrew Nyere, akiteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na kuvaa kofia ya Chama cha ACT-Wazalendo wakati viongozi wa chama hicho walipofanya ziara kijijini Mwitongo Wilayani Butiama. |