Mchaka Zaidi

Thursday, May 7, 2015

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA HATAGOMBEA TENA URAIS.

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2705586/highRes/1005433/-/maxw/600/-/d89d2d/-/pierre.jpgRais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewaambia mawaziri wa Afrika Mashariki kwamba endapo atachaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwezi June mwaka huu kwa muhula wa tatu basi itakuwa ni kipindi cha ukomo wa yeye kuendelea kusalia madarakani ,msemaji wa serikali ya Burundi Gervais Abayehorwa amesema hayo mapema Jumatano.



Rais Pierre Nkurunziza uamuzi wake wa kugombea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu uliibua hisia tofauti tofauti na kuzusha maandamano makubwa. Waandamanaji wanadai kwamba kwa muujibu wa katiba ya nchi hiyo rais anapaswa kuiongoza nchi kwa mihula miwili tu.

Nayo mahakama ya katiba wameeleza kwamba hawahesabu muhula wa kwanza wa raisi huyo madarakani kwasababu aliteuliwa na wabunge na si kuchaguliwa kwa kupigiwa kura.

Regina Mziwanda kutoka mjini Dar-Es-Salaam amezungumza na msemaji huyo wa serikali ya Burundi ,kutaka kujua Nini ujumbe wa Rais Pirre Nkurunziza kwa taifa la Burundi pindi alipohutubia mapema Jumatano.?

MTANDA BLOG

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.