Pambano la ngumi za kulipwa kati ya
Floyd Mayweathe na Manny Pacquia
limemalizika kwa Mmarekani Mayweather
kushinda kwa pointi sita dhidi ya mpinzani wake Mphilipino Pacquiao
baada ya pambano hilo kumalizika kama chati inavyoonyesha hapa chini.
Floyd ameibuka na pointi 117 alizopewa
na majaji kutokana na kurusha vyema makonde yake dhidi ya mpinzani wake
wakati Pacquiao yeye ameambulia pointi 111 zilizomfanya ashindwe
kuibuka mbabe dhidi ya Floyd.
Pambano hili limekuwa la kihistoriakwa
dunia nzima ililazimika kusubri kuona nani kati ya bondia Floyd ‘Money’
Mayweather na Manny Pacquiao ataibuka mshindi lakini kitandawili hicho
kimetenguliwa.
Pambano lilikuwa raundi 12, ambapo Floyd
Mayweather amefanikiwa kumshinda Pacquiao kwa pointi hizo sita tu na
kuamua mbabe kati yao ni nani.
MTANDA BLOG
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.