MSANII nyota wa filamu, Elizabeth Michael `Lulu’
amekanusha uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao
yanatokana na yeye kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea,
Amani linakujuza.
Akizungumza na Gpl juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusiana
na matukio mengi yanayomtokea, muigizaji huyo wa filamu ya Foolish Age,
alisema maisha yake ya siku hizi ni ya kusali sana, hivyo anaamini
kutokana na maombi yake, hali yake iko vizuri kutokana na Mungu kumpa
anachokihitaji.
“Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo mara tatu
kwa siku, ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka, hayawezi kukaa
mwilini mwangu,” alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita,
aliondokewa na mpenzi wake, Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki
mbele yake.
Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, Maalim Hassan Yahya
Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini mauti
ambalo baada ya kumpenda, halitaki kuridhia uhusiano wake wa kimapenzi
na binadamu.
“Hapa nimshauri tu, achukue hatua ya matibabu haraka
iwezekanavyo vinginevyo hali hiyo itaendelea, anatakiwa afanye kafara
kwa kuchinja mnyama yoyote ili aondokane na matatizo haya,” alisema.
CHANZO: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.