Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amesogeza mbele uchaguzi wa
wabunge kwa siku 10 hadi Juni 5 mwaka huu kufuatia jaribio la mapinduzi.
Msemaji wa Rais, Willy Nyamitwe ameliambia Shirika la Habari la AFP
kuwa kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliyopita na vurugu
zilizofuatia ni bora kusogeza mbele uchaguzi huo kwa muda.
"Uchaguzi huo wa wabunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika Mei 26 mwaka
huu lakini sasa inatubidi kuusogeza mbele mpaka Juni 5 mwaka huu ili
kuwasikiza washirika wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo
pia inatumia muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya
upinzani" alisema Nyamitwe.
Mpaka sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanywa Juni
26 mwaka huu bado haijabadilika na nia ya Rais Nkurunziza kuwania urais
kwa muhula wa tatu ipo palepale.
Chanzo:
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.