Mamlaka nchini Kenya imesema kuwa walinda usalama wamekabiliana na
washukiwa wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab, katika
wilaya ya Ijara katika kaunti ya Garissa Kaskazini Mashariki mwa nchi
hiyo.
Mapema, wapiganaji hao waliokisiwa kuwa zaidi ya 50 kutoka Somalia,
wanasemekana kushambulia kambi za polisi katika eneo la Yumbis, takriban
kilomita 30 kutoka Daadab.
Wavamizi wa Al-Shabaab waliteka vijiji vitatu na kupeperusha bendera
yao Kaskazini Mashariki mwa Kenya kwa muda kabla ya maafisa wa polisi
nchini kenya kuwasili na kuwatimua. Vijiji vilivyovamiwa ni Ramu iliyoko
Mandera, na vijiji vya Yumbis na Holugho vilivyoko Garissa.
Walioshuhudia wamesema kuwa wapiganaji hao waliikejeli serikali ya
Kenya na wakawaonya wanavijiji kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya
Kenya.
Japo viongozi nchini Kenya wamesema kuwa maafisa wa usalama
wamewafukuza wanavijiji wenyeji wa Yombis wanaodai kuwa bado wapiganaji
hao wako.
Chanzo:
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.