Sijawahi kuwa Mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo na sijafikiria kujiunga na chama hicho. Nilishawahi kuwa Mwanachama mtiifu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)
Nikiwa
ndani ya CHADEMA nimewahi shiriki katika harakati nyingi zote
zikiwa na lengo la kukikuza chama ambacho niliamini ndo
mkombozi wa kweli wa mtanzania.
Bahati mbaya sikuwa sahihi, nilikosea kukiamini chama hicho ambacho idadi kubwa ya viongozi wake ni mahafidhina.
Nikiwa
ndani ya siasa, nimefanikiwa kujuana na wanasiasa wengi wakubwa
kwa wadogo, mmoja wao ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto
Kabwe.
Namjua
Zitto, nafahamiana naye vizuri, ni mmoja wa wanasiasa wasomi,
wenye siasa safi ambaye mara zote kauli na hoja zake zimetaliwa
na busara na nia ya kulijenga taifa, siwezi kusema si
mbinafsi moja kwa moja lakini nina imani nae kubwa kuwa si
mbinafsi.
Zitto
ameweza kuzimudu siasa safi za taka zilizokuwa zikiendeshwa
ndani na nje ya chadema kabla ya kuhamia ACT- Wazalendo.Ameweza
kupambana na kupenya kwenye changamoto nyingi za kisiasa hasa
siasa hizi za kuwa na chama kimoja kikongwe na chenye nguvu
nchini na nje ya nchi.
Sote
tunaijua CCM ni chama chenye wanachama na viongozi wanaoijua
siasa, wanaweza kukibadili chama hicho wakati wowote, chama hiki
kikuu nchini ni kama kinyonga, kinabadiilika kulingana na
mazingira na wakati.
CCM
kinapanga vyema karata zake, kina propaganda zenye kuwiana na
ukweli tofauti na ilivyo kwa upinzani ambao wanadanganya
wananchi mpaka wanajidanganya wao wenyewe.
Zitto
ameweza kupenya kote huku na ndio maana leo hii, Zitto
anaposulubiwa hata CCM kinaumia na kumhurumia, kwa sababu
wanamjua mwanasiasa huyu kijana ni mtu wa namna gani.
Kama
si uimara wa Zitto huenda angeshaanguka maana wapo watu na
vyama vilivyotupwa nje ya siasa kutokana na kukosa misingi ya
mapambano ya siasa za aina zote.
Hata hivyo chadema kimefika hapo kilipo pamoja na mambo mengine mchango wa Zitto unahusika kwa kiwango kikubwa.
Katibu
mkuu wa chadema Dr. Wilbroad Slaa kwa kushirikiana na Zitto
walieweza kukifikisha chama hapo kilipo, hilo haliepukiki na
anayekataa ana chuki zake binafsi.
Zitto
akiwa mchanga kisiasa lakini mwenye maono alichanga karata
zake vyema, akashiriki kukitoa chama kutoka kuwa na wabunge 11
hadi kukifikisha hapa kilipo, ambapo leo kuna zaidi ya wabunge
40.
Historia
ya Chadema haiwezi kukamilika bila ya kumhusisha Zitto katika
mafanikio yake huku akipambana kwa karibu sana na Dr. Slaa, na
mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye kwa bahati mbaya amejikuta
akivurugwa na wapambe.
Chadema
ya Zitto akiwa kama Naibu katibu mkuu Bara, waliweza
kukidhibiti CUF na Hamad Rashid ambaye alikuwa kinara ndani ya
bunge.
CUF
ilikuwa na hoja dhaifu na mikakati isiyotekelezeka pamoja na
kauli mbiu za hatari za mapanga shaa,Interehamwe na Saigon.
Chadema
ya Zitto na Dr Slaa walikuwa wakitoa hoja zenye mashiko,
walikuwa moto mkali ndani ya bunge, hakuna aliyeacha
kuwasikiliza watu hao wanapopata nafasi ya kuzungumza.Bunge la
9 lilikuwa ni moto wa kuotea mbali.
Bunge
hilo lilileta mapinduzi makubwa ya kiungozi na kiutendaji
serikalini.Mikataba mibovu ilichambuliwa,Sakata la EPA iliiibuka,
mgodi wa Buzwagi nao ulipewa nafasi na masikini walipiganiwa.
Chama
kikanawiri na kushamiri hadi kufikia leo kuwa na wabunge 40,
ajabu ni kwamba baadhi ya viongozi wa chama hicho wamesahau
mema yote ya Zitto badala yake wanashiriki kwenye harakati
chafu za kumchafua.
Wanataka
kuiaminisha jamii kuwa Zitto ni Msaliti, kwamba anapaswa
kutukanwa, kusimangwa na kubezwa. Zitto huyu anayejua kupanga
karata leo hii amekuwa adui na msaliti wa chadema, chama
alichojiunga nacho akiwa kinda!
Dhambi
hii ya ubaguzi waliyoifanya Chadema itawarudia, hawatapona kamwe,
hawatabaki salama, wataparanganyika tu, nawaombea heri wasifike
huko ingawa dhambi ya ubaguzi haiishi.
Kama
nilivyotangulia kusema hapo juu, namjua Zitto, nimefanya nae
kazi ni mmoja wa waliokuwa viongozi kipenzi cha watu wa rika
na kada zote ndani ya chama hicho.
Alipendwa
naa viongozi wa ngazi ya chini Chadema, alikuwa ni mtu wa
kujishusha na kuwasikiliza viongozi waliochini yake.Hata kama
aliyoelezwa yalikuwa nje ya uwezo wake hakuyapuuza.
Tofauti
yake na viongozi wakubwa wa chadema, yeye alikuwa akifika
kwenye mikutano hata akute watu wachache hakuwa akiacha
kuhutubia na kuwapa moyo.
Alikuwa
akiyatumia mazingira hayo ya watu wachache kusimulia baadhi ya
visa vyake vya kisiasa, wakati huo ndo wanajenga chama.
Naamini
anakikumbuka kisa hiki, kwamba yeye na Mdee walikwenda mahali
na kukuta watu wachache.Hwakuacha kuhutubia, walihutubia, lakini
ajabu hao watu wachache waliokuwepo walikuwa wakiendelea na
harakati zao, wengi wao walikuwa wakinunua ndizi mbivu......Kwa
maana nyingine hawakuwa wakisikilizwa.
Alichokifanya
ni kumuomba Mdee akazinunue zile ndizi zote ili watu wakose
cha kununua na badala yake wageuke kuwasikiliza.
Hata
hivyo, mpango wao huo haukufanikiwa, kwani kila mtu aliyekuwa
pale aliendelea na mambo yake. Chakufurahisha Zitto na Mdee
hawakukata tamaa, walipambana kuwashawishi watu wakielewa
chama.Leo hii chama kikifika eneo lile lile watu wanakanganyana
ili kumsikiliza kiongozi wa chama anayezungumza hata kama
anaongea pumba.
Zitto
alikuwa mtu wa kujichunga sana katika matamshi yake, hakuwa
akiongea bora aongee, alikuwa akiongea yanayopaswa kuongelewa kwa
wakati huo na kwa wakati stahiki.
Mwandishi: Joseph Yona ( 0713802226)
Chanzo: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.