KAMATI ya Ukweli na Maridhiano ya Chama cha Tanzania Labour (TLP),
imetangaza kumvua uanachama Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino Mrema.
Akizungumza jana, jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joram Kinanda alisema kuwa kamati hiyo
imefikia uamuzi huo baada ya kupitia kwa kina malalamiko yaliyokuwa
yakimuhusu Mrema, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mbali na Mrema wengine waliovuliwa
uanachama ni Hamisi Mkadamu, Antoni Mapunda, Nancy Mrikaria, Dominata
Rwechungura, Maxmilian Lymo, Richad Lyimo, Hamisi Mkumba na Stanley
Temba.
Kinanda alisema kuwa wanachama hao wamevuliwa uanachama kwa
mujibu wa katiba ya chama hicho, toleo la 2005 Ibara ya 9.9 (c) na 2009
ibara 9.5(c).
Kinanda alisema kuwa maazimio hayo yamepelekwa katika ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa kwa taratibu za kisheria pamoja na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa nchini, Sisty
Nyahoza, alipotafutwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema kamati
hiyo haitambuliki kisheria.
“Kamati hiyo haitambuliki kisheria, na hata Mrema mwenyewe amekuwa
akipinga TLP kuwa na kamati ya aina hiyo na hata viongozi wake
hawatambuliki, ” alisema
CHANZO: Mtanzania na Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.