Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa
Tanzania ambaye pia ni baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ajulikanaye
kama Makongoro Nyerere naye anatarajia kutangaza nia ya kugombea urais
katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari
imebainisha kuwa Makongoro Nyerere atatangaza nia ya kugombea urais
kupitia chama cha Mapinduzi ifikapo tarehe moja mwezi wa sita mwaka huu
yaani siku ya jumatatu.
Makongoro nyerere ameungana na Waziri Prof. Mark Mwandosya ambaye
naye anatarajia kutangaza nia siku ya jumatatu huku waziri mkuu wa
zamani Edward Lowassa akitangaza kutangaza nia siku ya jumamosi ambayo
ni mei 30 mkoani Arusha.
Chanzo: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.