Maelfu
ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wameanza
mgomo kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu kwa
zaidi ya wiki 11 huku wakitaja gharama za maisha zikiwa zimepanda mara
dufu.
Wakiongea
katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam kwa kile
walichokiainisha kuwa ni njaa kali pamoja na kueleza kuendelea na mgomo
hadi fedha zitakpoingia kwenye akaunti zao wametaja serikali
kuchelewesha fedha hizo kupitia bodi ya mikopo kuwa ni kuwadhoofisha
kimasomo.
Kwa
upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza
Mukandara pamoja na kukiri madai ya wanafunzi elfu saba kati ya zaidi ya
elfu kumi wanaofadhiliwa na serikali kupitia bodi ya mikopo
kucheleweshewa fedha zao kuwa ya msingi,amesema tayari amezungumza na
bodi ya mikopo ambao wamemwahidi kuleta fedha zao haraka iwezekanavyo na
kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.
Wakati
huohuo takribani wanafunzi 400 wa chuo kikuu cha Mt. Josephu cha Mbezi
jijini Dar es Salaam mwaka wa kwanza wamesimamishwa masomo kwa muda
usiojulikana baada ya kugoma kuingia madarasani wakidai fedha za kujikim
kutoka bodi ya mikopo tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi sasa
wakieleza kuishindwa kuendesha maisha yao ya shule na kuhimili mazingira
ya kupanga nyumba mitaani.
Katika
taarifa ya kusimamishWa wanafunzi hao iliyotolewa na makamu mkuu wa
chuo cha Mt.Josephu Bw.Loyola Proteep aliyeambatana na mkuu wa wanafunzi
maarufu kama Dean anakiri madai ya wanafunzi hao kuwa ya msingi na
kuongeza kuwa waliwaomba utulivu na kuingia Madarasani wakati
wakifuatilia madai yao bodi ya mikopo bila ya mafanikio na uongozi
kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza hadi
vikao vya bodi vitakapoamua vinginevyo.
CHANZO:
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.