HUDUMA za kijamii mkoani Mtwara jana zilisimama kutokana na baadhi ya wananchi kudai kuwa wanaomboleza vifo vya watu vilivyotokea wakati wa vurugu za gesi hivyo kupelekea huduma za kijamii kusimama.
Mmoja
wa wananchi walioathiriwa na mgomo huo, Hilal John aliyekuwa safarini
kuelekea Newala lakini alikosa usafiri kutokana na kumbukumbu hiyo
alisema hatua hiyo imeathiri wananchi wa hali ya chini.
Alisema
hali hiyo imesababisha wasafiri wanaokwenda wilaya zote pamoja na
baadhi ya mikoa kushindwa kuondoka kutokana na kutokuwepo kwa huduma
hiyo kwa siku nzima ya jana.
Si hivyo tu, maduka mbalimbali nayo yalifungwa na hivyo kusababisha baadhi ya watu kukosa huduma hizo.
“Nimi
nilikuwa naelekea Newala kwenye usaili lakini nimeshindwa kwenda hadi
muda huu niko kituoni hakuna hata dalili ya magari zaidi ya mabasi ya
kwenda Dar es salaam ndio yapo, hii inatufanya tushindwe kuelewa kwanini
huu mgomo unafikia hatua ya kusimamisha safari na huduma muhimu za
kijamii” alihoji John
Kwa
upande wake Fatuma Halfani anayemiliki mgahawa katika kituo cha mabasi
alisema mgomo huo kwa sehemu kubwa umeathiri akina mama lishe ambao
wamekuwa wakitegemea biashara hiyo kuendeshea maisha yao.
Alisema amekuwa akifanya biashara hiyo kwa muda lakini analazimika kupata hasara kutokana na mgomo ulipo ili kuepuka vurugu .
Halfan
alisema kitendo cha wananchi kuweka maombolezo ya mgomo kwa huduma za
kijamii ambazo ni muhimu zinazowagusa wananchi wa hali ya chini ni jambo
la kusikitisha kwa kuwa wananchi wa hali ya juu wanaendelea kupata
huduma hizo.
Naye
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mtwara George Salala alisema Mtwara ipo katika
hali ya utulivu hivyo kuwataka wananchi kuendeleza amani iliyopo na
kuwaonya wachache ambao watajaribu kufanya vurugu ambazo zitasababisha
uvunjifu wa amani.
Alisema
Jeshi la polisi linawataka waliokata leseni kwaajili ya biashara
wafanye biashara na kwa watoa huduma sokoni wafungue maduka kwa kuwa
hawatakusudia kuwachokoza kwa kuwa wao ni serikali na zaidi ofisi zote
za serikali zilikuwa zikifanya kazi kama kawaida.
“Sisi
kama jeshi la polisi hatuko tayari kuona watu wanaingilia uhuru wa watu
wengine hatutasita kuwachukulia hatua na kuwafikisha mbele ya sheria
tunaitaka jamii ione madai hayo kama hayana tija ili tuweze kusonga
mbele lakini hatuwezi kusonga mbele” alisema Salala
Chanzo: Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.