Mchaka Zaidi

Monday, May 25, 2015

Mfahamu Zaidi Mwigizaji Rose Ndauka....Wapi Alitoka, Lini Alianza Sanaa na Mengine Mengi Kuhusiana na Maisha Yake


Anafahamika zaidi kama Rose Ndauka ni mmoja warembo wenye mvuto wa pekee ndani ya tasnia ya bongo movies kwa vipaji vyake vingi sana. 

Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia ose ni mwandishi na mwongozaji wa Filamu. 
 
Akiwa ameshaigiza kwenye zaidi ya Filamu kumi na saba (17) na kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ya best actress in mini ziff 2011; Rose Pia ni mfanyabishara na anamiliki kampuni yake binafsi iitwayo Ndauka Entertainment inayojihusha na mambo ya Filamu na burudani. 
 
Rose Hupenda kusikiliza muziki, kuogelea, na  kusoma vitabu akiwa yupo nyumbani  

Historia ya Rose inaanza tarehe saba (7) mwezi wa kumi (10) mwaka 1989. Huu ni mwaka tarehe na siku alipozaliwa. 
 
Alizaliwa hapa hapa Tanzania na kupata elimu yake katika shule ya sekondari zanaki- Dar es salaam . Toka alipokuwa mdogo sana Rose alipenda kuigiza.
 
Kipaji chake Kiligunduliwa na mama yake mzazi kabla ya yeye mwenyewe kuamua kujiingiza rasmi kwenye tasnia ya Filamu nchini.

Rose alionekana kwa mara ya kwanza kwenye Filamu ya “SWAHIBA” aliyoigiza kama “Aisha” mnamo mwaka 2007. Filamu hii ilipigiwa kura kama Filamu bora ya mwaka na kituo cha redio cha clouds FM.
 
Baada ya Filamu hiyo Rose aliweza kupata nafasi ya kuigiza katika Filamu mbalimbali zikiwemo Mahabuba na Solemba na nyota yake ilionekana sana pale alipoigiza Filamu ya Deception na marehemu Steven Kanumba kama mmoja wa waigizaji wakuu pamoja na Lost Adam aliyoigiza na mkali mwingine wa bongo movies Jacob steven “JB”
 
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya “Ndauka Entertainment”  na pia alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu inayohusu mauaji ya halaiki ya Rwanda iliyopewa jina la “RWANDA BAADA YA VITA” ama (URWANDA NYUMA U’GENOCIDE)  kwa kirwanda.
 
Mwaka huo huo chini ya kampuni yake Rose alitoa filamu mbili za “BAD GIRL” na “THE DIARY” ambazo zilifanya vizuri sana sokoni.
Mashabiki wake wanapenda kuita “Rosie” na mara nyingi amekuwa akipata “attention” kubwa kwenye vyombo vya habari na magazeti kutokana na mvuto wake na umbo lake zuri.
Chanzo: Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.