Mchaka Zaidi

Sunday, May 24, 2015

Jeshi la Wananchi lazua kizaa zaa songea


Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani Songea jana limezua kizaa zaa kwa wananchi kufuatia kuvamia mitaani, maofisini (serikali na binafsi) makanisani na misikitini wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza upekuzi  kwa watu wote walokutana nao huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.

 
Aidha,indaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mjini hapo waliamua kujifungia ndani huku wengine wakisema kwamba jeshi hilo linawasaka  magaidi waliovamia katika mji wa Songea kutokana na jeshi hilo kutowafahamisha wananchi nini hasa dhumuni la msako huo.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida  huku akiwataka wakazi wa mjini songea  kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.
 
Naye  Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao na kuongeza kuwa  jeshi hilo  hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.
Chanzo: Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.