Licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani Zlatan Ibrahimovic pia amekumbana na aina ya swali ambalo linatafsirika ni sawa na kuulizwa kati ya Messi naRonaldo nani bora… Zlatan akiwa katika kipindi cha mahojiano alitakiwa kujibu kwa maneno yasiyozidi mawili atakapotajiwa jina la mchezaji yoyote.
Mtangazaji wa kipindi hicho Maggie Gray alianza kwa kutaja jina la Messi na Zlatan akajibu kwa neno moja tu “Fantastic” na alipotajiwa Ronaldo akasema “good” na mwishoni alipotajiwa jina lake alijibu “waoo”
Kwa majibu hayo, amemaanisha Ronaldo yuko vizuri ila Messi ni Fantastic yani uwezo wake ni mkali zaidi, nimekuwekea video ya namna Zlatan alivyojibu
Chanzo: Millardayo.com
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.