Klabu ya soka ya Simba imezidi kuimarisha kikosi chake kwa kuwasajili nyota kadhaa msimu huu… Simba ambayo ipo visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara inajipanga kurejesha heshima ya kikosi chake ambayo siku za karibu kimekuwa hakifanyi vizuri.
Baada ya kumsajili nahodha wake wa zamani Musa Hassan Mgosi sasa imemrejesha mkongwe mwingine Mwinyi Kazimoto aliyeondoka miaka miwili iliyopita na kutimkia Al Markhiya ya Qatar…Mwinyi amejiunga na Simba kama mchezaji huru na amesaini mkataba wa miaka miwili.
Ikumbukwe kuwa Mwinyi amewahi kuichezea Simba akitokea JKT Ruvu mwaka 2011-2012 kabla ya mwaka 2013 kutimkia Al Markhiya ya Qatar.
Chanzo: Millardayo.com
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.