Mchaka Zaidi

Tuesday, July 28, 2015

Mbunge Mwingine wa CHADEMA Arudisha Kadi na kujiunga na CCM


MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere ameng'atuka rasmi jana katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia alisema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

Alisema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
 
“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia” amesema Leticia.

Leticia alisema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.

Alisema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi.

Chanzo: Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.