Mchaka Zaidi

Wednesday, July 29, 2015

Rasmi Arturo Vidal amejiunga na timu hii….

Vidal1


Baada ya kuwa na uvumi kwa muda mrefu kuhusiana na mchezaji wa kimataifa wa ChileArturo Vidal anaekipiga katika klabu ya Juventus ya Italia kuhama, July 28 imekuwa ni mwisho wa uvumi huo. Vidal ambaye amekuwa akitakiwa na vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Manchester United, amemaliza uvumi huo.
Arturo_Vidal_(Juventus)
Vidal amesaini July 28 katika klabu ya FC Bayern Munich kwa mkataba wa miaka minne hii ikiwa ni ishara ya kumaliza uvumi wa mchezaji huyo kuwa angecheza wapi msimu ujao….Vidal amesaini mkataba huo mara baada ya kufanyiwa vipimo vya afya asubuhi ya July 28.
vidal
Mkataba huo utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2019. Bayern ilikuwa inahitaji huduma ya Vidal toka mwaka 2011 akiwa katika klabu ya Bayer Leverkusen na baadae kutimkiaJuventus ya Italia. Vidal amesajiliwa kwa dau linaltajwa kufikia pound million 28.
Chanzo :Millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.