“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje” >>>> Hii ni moja ya sentensi ambazo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM.
CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na headlines nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA.
Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae.
‘UKAWA tunahitaji viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa… Tunamwalika Edward Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuhakikisha tunaing’oa CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.. Tunaamini ana uwezo wa kuhamasisha umma kuikataa CCM na udhalimu wake‘ >>>>James Mbatia.
Zimeandikwa stori nyingi kuhusu Mbunge huyo kujiunga CHADEMA, kingine kilichoibua maswali mengi ni ishu ya UKAWA kuchelewesha kumtaja Mgombea wao wa Urais… hapa ziko picha mbili zilizoenea Mitandaoni zikimwonesha Mbunge Edward Lowassa pamoja na Viongozi wa UKAWA, kuna chochote kinafuatia?
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.