Mchaka Zaidi

Thursday, August 6, 2015

Breaking News: Lipumba Ajiuzulu Uenyekiti Wa CUF....Adai UKAWA Wameshindwa Kusimamia Makubaliano


MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.


Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania  katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).


Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA) wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.


Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).


Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa  kesi ya kufanya maandamano bila kibali.

Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu  pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.
Chanzo: Mpekuzi blog

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.