Mchaka Zaidi

Monday, August 10, 2015

Mambo matano ya Jerry Silaa uliyoyakosa wiki hii.

Jerry Silaa

Jumamosi ya 1/8/2015 baadhi ya mitandao na Magazeti kuliripotiwa kwamba Jerry Silaa ameshindwa kwenye kura za maoni jimbo la Ukonga lakini saa kadhaa baadae Mkurugenzi wa uchaguzi alitangaza Silaa ndio mshindi kwa kupata kura elfu kumi huku anaemfatia akipata kura elfu saba mia tatu arobaini na sita.
  1. Kwenye sentensi ya pili anasema >>> ‘Baadhi ya Wagombea hawakufata maadili, walikua wanaleta Wapambe na wengine wanafanya zile staili za kizamani kabisa za kwenda kata kwa kata na kuita watu na kugawa fedha, ni kinyume na maadili ya chama, dini na nchi
  2. Jerry Silaa anasema ni kweli kwenye jimbo langu Wagombea wote takribani 16 walikua wanafahamu kwamba mwenzetu Ramesh Patel Mtanzania mwenye asili ya Asia alikua anaongozana na Wapambe wengi, pia kila tunapokwenda kwenye kituo cha kesho, yeye leo usiku anapita kwa ajili ya kushawishi watu na ninazo msg
Ramesh
4. ‘Kwa haki ya mwenyenzi Mungu sijampa Mwanachama wa CCM hata shilingi moja kunichagua, nilikua nawaeleza tu kila kata na kuwaambia kwamba nilipokua Meya, Diwani mradi huu nimefanya kwa niaba ya Wafadhili na mradi huu nimefanya kwa niaba ya yangu binafsi au Halmashauri’ – Jerry Silaa.
Jerry Silaa 2
5. Anaendelea kwa kusema ‘Ilipofika Tarehe 27 Jumatatu alifanya vitendo hivyo kwenye kata ya Pugu Stesheni na Pugu Kajiungeni ambazo tulikua tunakwenda kuziona Jumanne, maafisa wa TAKUKURU walivamia mkutano ule na wakakamata watu akiwemo yeye na kuwatia mbaroni, naamini sheria itachukua mkondo wake.
Unaweza kumsikiliza Jerry Silaa hapa chini na chini yake pia kuna sauti ya TAKUKURU wakizungumza kuhusu kuwakamata Ramesh na wenzake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.