Mchaka Zaidi

Monday, August 10, 2015

Lowassa kuiamkia NEC leo + Siri ya Lipumba kuondoka CUF yafichuka + Maamuzi magumu ya UKAWA? >>Stori Kubwa (Audio)

ioo

Uchambuzi wa magazeti redioni umekupita? Nimefanya jitihada ya kukusogezea zile zote kubwa kubwa zinazoweka vichwa vya habari kwenye magazeti asubuhi hii zikiwa na baadhi ya hizi kubwa…
Joto la uteuzi wa Ubunge CCM lazidi kupanda jijini Dodoma…siri ya Prof. Imbrahim Lipumba kutoka CUF yafichuka, mipango ya Edward Lowassa yaivuruga CCMCCM yabomoka zaidi, wanachama 100 wajiunga CUFUKAWA yafanya maamuzi magumu na TAKUKURU yajingo’a meno.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa asema CCM haitishwi na watu wanaohama Chama hicho na hakiwezi kuendeshwa na vitisho hivyo na kitaendelea kushika dola.
Edward Lowassa kuchukua fomu ya ugombea Urais leo kwenye makao makuu ya NEC asema wapinzani wakiikosa nchi mwaka huu watasubiri miaka 50 huku akiituhumu CCM kwa kuwa wadau wa kuiba kura.
Prof. Ibrahim Lipumba aibukia Kigali asema UKAWA wamefanya uchaguzi kuwa wa CCM (A) dhidi ya CCM (B)...na Rais Jakaya Kikwete azindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio Mtwara.
Sauti ya uchambuzi wote wa magazeti @Cloudsfm nimekurekodia na kukuwekea hapa chini.

Chanzo: millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.