Mchaka Zaidi

Friday, August 7, 2015

Baba Levo na safari ya Udiwani wake Kigoma imefikia hapa..

Baba Levo

2015 Historia inaandikwa Tanzania kwenye Siasa, Vijana wengi wamehimizwa kuingia kwenye Kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi na wameitumia vizuri nafasi hiyo… Wasanii wako kwenye headlines, wapo waliofanikiwa kupenya kwenye hatua za mchujo wa kwanza na wapo ambao Kura hazikutimia pia.
Staa wa Bongo Fleva na comedy pia, Baba Levo aliaga Dar es Salaam kwamba anahamishia nguvu Kigoma kwa ajili ya Kugombea Udiwani kupitia Chama cha ACT- Wazalendo ambacho kinaongozwa na Zitto Kabwe.
Baba Levo amesema waliogombea kupitishwa nafasi hiyo walikuwa sita lakini wanne walijitoa na walibaki wagombea wawili tu kwenye hatua ya mwisho ambao ni Baba Levona Mzee Manyoni… Kwenye jumla ya Kura 67, Mzee Manyoni alipata Kura 20 na Baba Levo alipata Kura 47, Ushindi uko kwake na anasubiri Uchaguzi wa October 2015 ili kama akipita hapo basi awe tayari kafikia kilele cha safari yake kwenye Udiwani.
Hii ni post ambayo kaiweka kwenye ukurasa wake @Instagram, yuko na watu wake mtaani wanashangilia hivi..
Chanzo: Millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.