Saturday, April 25, 2015
Polisi Anusurika Kuuawa na Wananchi Wenye Hasira Kali Mkoani Morogoro jana Mchana
Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria,
aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika kuuawa leo (jana) mchana na wananchi
wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva
wa bodaboda ambaye aliparamia lori.
Afande Sele: Nikichaguliwa Kuwa Mbunge Nitakataa Posho na Mishahara Mikubwa
Mwana hip hop na Bongo Fleva nchini, Afande Sele, ameweka wazi kwamba
hata kama atakuwa mwakilishi wa wananchi katika bunge la mwakani,
hataweza kuacha kufanya muziki kwa kuwa ndiyo njia ya kumuingizia
kipato.
CCM Wamjibu Dr. Slaa Kuhusu NEC......Wakanusha Kukisaidia Chama Kipya Cha ACT-Wazalendo
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,
amekanusha madai yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, kwamba Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imeanza kuandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
katika ngome za CCM na kueleza kuwa huo ni upotoshaji mkubwa kwani
Tanzania nzima ni ngome ya chama hicho.
Wednesday, April 22, 2015
Breaking News: Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola
Habari zilizotufikia zinaarifu kuwa basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.
Mapambano Bado Yanaendelea......Jana CHADEMA na ACT-Wazalendo Nusura Wakutane Uso Kwa Uso Nyumbani Kwa Baba wa Taifa. Vurugu Za Mnyika Ziligonga Mwamba Kwa Mara Nyingine
Mtoto wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Andrew Nyere, akiteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na kuvaa kofia ya Chama cha ACT-Wazalendo wakati viongozi wa chama hicho walipofanya ziara kijijini Mwitongo Wilayani Butiama. |
Mambo Yameiva: Mmiliki wa Gombe high School, Dkt Yared Fubusa Atangaza Nia Ya Kugombea Ubunge Jimbo La ZITTO KABWE Kwa Tiketi ya CHADEMA
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Gombe school of Environment and Society (GOSESO) na mmiliki wa Gombe high school, Dkt Yared Fubusa ambaye pia ni kada wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ametangaza nia ya kugomba ubunge jimbo la Kigoma kaskazini kupitia chama hicho.
Subscribe to:
Posts (Atom)