Mchaka Zaidi

Monday, March 23, 2015

BAADA YA KUTUA ACT,AFANDE SELE ATANGAZA NIA

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, Suleimani Msindi ‘Afande sele’, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa Morogoro mjini kupitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).


Msanii huyo ametangaza azma yake hiyo jana mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


“Niliumizwa baada ya kusikia kuwa eti katiba ya chama inasema kuwa mwanachama anayekwenda mahakamani kudai haki yake anakuwa amejivua uanachama wake.


Kwa chama kama Chadema sikuamini kama kingekuwa na sheria kandamizi kama hiyo ya kuzuia wanachama wake kwenda mahakamani, ambacho ndicho chombo cha mwisho kwa mtu kudai haki,” alisema.


Akielezea sababu nyingine iliyomfanya kujitoa Chadema imechangiwa na kuondolewa kwa Zitto Kabwe, ambaye alichangia kumhamasisha kujiunga na chama hicho.


“Jambo jingine nililojiuliza ni kwamba kama mti mbichi (Zitto), umetendwa hivyo je, mimi mkavu itakuwaje nikaona bora nivue ukamanda nivae utaifa kwanza,” Alisema Afande Sele

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.