Mchaka Zaidi

Tuesday, March 31, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 31 March 2015



Kaka Yake Gwajima Amtaka Amuombe Radhi Pengo.



Kaka wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aitwaye Methusela Gwajima amemtaka mdogo wake kwenda kumuomba radhi Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo kwa kutoa lugha ya kumkashifu.
 

Watu Watano Wajeruhiwa Vibaya baada ya Kuangukiwa na Kifusi Cha Ukuta wa Jengo la Ghorofa 7 Jijini Mwanza.



Watu watano katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza wamenusurika kifo baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye maandalizi ya kujenga jengo lililotegemewa kuwa na ghorofa saba, eneo la Nyerere Road,   jana majira ya saa sita mchana.
 

Sunday, March 29, 2015

Urais 2015: Lowassa Aongoza, Mwingulu Nchemba Ang'ara Kama Kijana Anayekubalika Zaidi.



Taasisi isiyo ya kiserikali ya Positive Thinkers Tanzania imetoa ripoti yake ya utafiti kuhusu mwanasiasa anayekubalika zaidi na wananchi katika nafasi ya Rais ajaye.

Zitto Kabwe Achaguliwa Kuwa Mkuu wa Chama cha ACT-Tanzania.



Kiongozi mpya wa chama cha ACT Tanzania, Zitto Kabwe akionyesha alama ya chama ambayo ni "Uwazi" baada ya kuchaguliwa.

Abdul Bonge, Mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection Afariki Dunia



Aliyewahi kuwa Meneja wa wasanii na mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge amefariki dunia 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Tarehe 29 March 2015



Hali ya Gwajima Bado ni Tete......



Wakati hali ya kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, ikiwa tete kwa siku mbili mfululizo, Jeshi la Polisi na waumini wa Askofu huyo wanadaiwa kuvutana hospitali inayofaa kumpa matibabu.

Rais Kikwete Atoa Msimamo wake Kuhusu Mahakama ya Kadhi......



RAIS Jakaya Kikwete amefafanua msimamo wa Serikali katika mjadala unaoendelea wa Mahakama ya Kadhi, na kuweka wazi kuwa Serikali haina mpango wa kuianzisha, wala kuiendesha.
 

MHHHHHH!!!!!! ILA..... Soma magazeti ya leo Jumamosi ya Tarehe 28 March 2015




Saturday, March 28, 2015

Gwajima Azimia Akihojiwa Polisi.....



Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
 

Baada ya Kuzimia, Akizinduka Askofu Gwajima Atakiwa Kuripoti kwa ...........




Wakati  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akijisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka alipoti ofisini kwake kesho kutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.

UKAWA: Ikulu Hiyo 2015......Wakubaliana Kuweka Mgombea Mmoja Kila Jimbo.



Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema kila chama ndani ya umoja huo kiko huru kutoa fomu na kuandaa wanachama wake watakaoshindanishwa katika mchakato wa kuwapata wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
 

‘Gaidi’ wa Mapangoni Amboni Tanga Atiwa 'Mbaroni'



JESHI la Polisi mkoani Tanga, limedai kufanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa aliyehusika kwenye tukio lenye sura ya kigaidi katika mapango ya Amboni.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Yabaini Madudu Makubwa Serikalini.......Rais Kikwete Atoa Maagizo Makali!!



Rais Jakaya Kikwete amekabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka unaoishia Juni 2014 na kuagiza vyombo vya dola kuwabaini maofisa wote wa Serikali wanaohusishwa na matumizi mabaya ya fedha za umma, ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Friday, March 27, 2015

Mchungaji Gwajima Ajisalimisha Polisi Kuhojiwa Juu ya Lugha Chafu Dhidi Ya Askofu Pengo.



Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Soma Habari za Magazeti ya Leo Ijumaa ya Tarehe 27 March 2015.




Lady Jaydee nae Mhhhhhhh hii kali

Lady Jaydee haogopi kufa na infact anataka mazishi yake yawe na mwaliko kama vile harusi zilivyo.

Afya Mama Yake Diamond Bado si Nzuri

Afya ya mama mzazi wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz, Sanura Kassim ‘Sandra’ bado si shwari juzikati hali yake ilibadilika ghafla na kuilazimu familia yake kumkimbiza katika Hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini Dar ambako amepewa kitanda.

Afumaniwa Gesti na Mume wa Dada Yake

Binti aliyetajwa kwa jina la Biena mkazi wa Kawe jijini Dar, hivi karibuni alipata aibu baada ya kufumaniwa ndani ya gesti (ipo maeneo hayohayo) akiwa na mume wa dada yake.

Rwanda kushirikiana na Tanzania - Kagame

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema serikali yake itashirikiana na Tanzania pamoja na nchi nyingine zinazounda ukanda wa kati wa maendeleo, ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa reli ya kisasa inayounganisha nchi hizo unakamilika.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Nchini Afutiwa Dhamana

Mahakama mkoani Dodoma imefuta dhamana ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa ikiwemo ya kutowazuia wafanyabiashara kufunga maduka yao wakati kesi yake ikiendelea mahakamani

Vijana wengi hawana nguvu za kiume.

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),imesema vijana wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea, wanaongoza kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.
 

Thursday, March 26, 2015

KUHUSU LOWASSA....CCM Arusha Watoa ONYO Kali kwa Nape Nnauye.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) MKoani Arusha, Robson Meitinyiki, amemtaka Katibu wa halmashauri Kuu (Nec) Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuchunga kauli zake dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Baada ya Askofu Gwajima Kumtukana Askofu Pengo, Polisi Wamtaka Ajisalimishe Kituo cha Polisi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

Wednesday, March 25, 2015

UKUTA WA NYUMBA YA DIAMOND WAANGUKA YAHUSISHWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.


Siku chache zilizopita Diamond aliamua kuweka picha za nyumba yake mpya aliyohamia na wengi walimpongeza kwa kujenga nyumba ya kifahari kama hiyo. Mpya zilizotufikia leo ni kuhusu kuanguka kwa ukuta wa mbele wa nyumba yake.

Baada ya watu wengi kuiona picha hiyo mtandaoni wengi waliihusisha na ushirikina wakiamini kua maadui wa Diamond watakua wamefanya fitna hadi ukuta huo kuanguka. Huku wengine wakisema kua hakuna ushirikina bali ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa jijini Dar.

CCM YAMUONYA TENA EDWARD LOWASSA,.....KUHUSU!!!!!!


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema vitendo vinavyofanywa na Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ni ukiukwaji wa Katiba na kanuni za chama hicho. 


Aidha, kimesema vitendo vinavyofanywa na Lowassa ni kampeni za wazi za urais anazoendesha kabla ya muda kufika na hivyo kukiuka Katiba na kanuni za CCM na kuonya kuwa kama ataendelea na kampeni hizo haramu atapoteza sifa za kugombea nafasi ya urais.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitoa ufafanuzi huo baada ya waandishi wa habari waliopo katika msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutaka ufafanuzi wa kinachoendelea mjini Dodoma kwa makundi tofauti kwenda kwa Lowassa kwa madai ya kumshawishi agombee urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 



Nape akizungumzia suala hilo alisema, “Anachokifanya Lowasa ni kuvunja kanuni na kiburi, ni matendo ya wazi ya kampeni, bila shaka anajua adhabu yake. Matendo hayo yanaweza kumpotezea sifa za kuwa mgombea kupitia CCM.”

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa aliongeza kuwa Lowassa ni miongoni mwa wanaCCM ambao walipewa adhabu na CCM mwaka mmoja uliopita kwa kuanza kampeni kabla ya wakati na mpaka sasa bado wapo kwenye kipindi cha uangalizi wakati vikao husika vikiendelea na tathmini dhidi yao.

Nape alisisitiza kuwa matendo yanayoendelea hivi sasa ni dhahiri kuwa ni kiburi kisicho na maana dhidi ya CCM.

“Lowasa anajua utaratibu wa Chama katika kuwapata wagombea wake kwa ngazi mbalimbali kuanzia udiwani mpaka urais hivyo kuendelea na matendo ambayo yanatafsiri ya wazi kuwa ni kampeni ni kiburi cha wazi. “Kwa matendo hayo ya Lowassa labda dhamira iwe ni kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama kingine na si CCM.”

Nape alisema ni vyema wagombea wa ngazi mbalimbali wakahakikisha wanazingatia Katiba na kanuni za chama hicho ili wasiingie kwenye kundi la kutokuwa na sifa ya kuomba ridhaa ya kugombea udiwani, ubunge na urais.

“Tunaendelea kukumbusha na kusisitiza kwamba wale wote wenye nia ya kugombea kupitia chama chetu kuheshimu kanuni na tararibu za kupata ridhaa kugombea kwa ngazi ya chama chetu,” alisema Nape.

Lowassa amedaiwa kuwa amekuwa akitumia makundi mbalimbali kufanya kampeni ambapo alianza na kikundi cha wajasiriamali jimboni Monduli mkoani Arusha ambapo walienda nyumbani kwake kumuomba agombee.

Hatua hiyo ilifuatiwa na mashehe 50 kutoka wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambao nao walikwenda nyumbani kwa Lowassa Dodoma kwa lengo la kumshawishi agombee urais.

Baadaye walifuata wachungaji ambao nao walifunga safari hadi nyumbani kwa Lowassa Dodoma na kusema wameamua kumuomba Lowassa agombee urais kwa madai kuwa ana maono makubwa dhidi ya Tanzania.

Baadhi ya wachungaji hao walimwambia Lowassa wanaamini kuwa yeye ndio chaguo sahihi kwao na ndio maana wameamua kufunga safari na kumshawishi huku wakieleza kuwa kila mtu ametumia nauli yake kufika Dodoma.

Kwa upande wake Lowassa, akizungumza na wachungaji hao waliofika nyumbani kwake, alisema anafarijika kuona makundi mbalimbali yakifika nyumbani kwake kumshawishi agombee.

Alinukuliwa na vyombo vya habari juzi akisema pia kuwa hakuna kundi ambalo analituma au kulipa fedha kwa ajili ya harakati za kutaka kugombea urais.

Hata hivyo, tayari baadhi ya makada wa CCM ambao wamo kwenye orodha ya kutaka kugombea urais, wametoa malalamiko yao kuwa kinachofanywa na Lowassa si sahihi.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema kuwa kitendo cha kuandaa watu kwa ajili ya kuanza kampeni si cha kiungwana na kwamba kila mgombea anaweza kufanya hivyo, lakini wanaheshimu kanuni na Katiba za chama chao.

January amenukuliwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii akieleza wazi kuwa anaweza kutengeneza makundi kwa ajili ya kuonesha Watanzania kuwa anahitajika, lakini akasema hizo ni propaganda ambazo hazina tija kwa Taifa.

"Kama mgombea anakubalika kwa Watanzania kwanini atumie fedha nyingi kutafuta makundi ili aonekane anakubalika? Alihoji January katika ujumbe wake aliousambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii"
.HABARILEO

Monday, March 23, 2015

MR UKIZIONA DALILI HIZI KWA KIPENZI CHAKO UJUE UMEACHWA

Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo kuficha mawazo yake.

Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.

Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.

Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.

KUPENDA KUJITENGA 
Mwanamke ambaye anapenda kujitenga na mpenzi wake atakuwa kwenye hatua za awali za kuelekea kuachana naye. Tabia ya mwanamke kutopenda kukaa karibu na mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara ya kuchoka au kukinai penzi. Hoja inabaki pale niliposema pa yeye kushindwa kuamua haraka na hivyo kutengeneza kwanza hali ya kumpuuza mpenzi wake.

KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Mwanamke ambaye hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi wake yuko kwenye hatua za kuacha. Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria utoshelevu wa kihisia ambao ndiyo unaoelezwa kuwa ni muhimu kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko kitu kingine chochote.
Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.


KUPENDA KUKOSOA
Kama nilivyosema, kujua historia ya penzi lenu namna lilivyoanza ni jambo muhimu kwa sababu husaidia kujua kama kuna mabadiliko hatari ya tabia za mwanamke.
Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.

UHUSIANO NA MTU MWINGINE
Licha ya kwamba usaliti kwenye uhusiano limekuwa suala la kawaida siku hizi, lakini mwanamke ambaye atakuwa hafichi uhusiano wake wa pembeni na kuacha minong’ono ikikufikia huku yeye akionesha kutojali malalamiko yako ya kusalitiwa, ujue hiyo ni ishara kwamba mwanaume wa pembeni amemfikisha kwenye hitaji la moyo wake na hivyo kuachana na wewe si jambo la gharama kwake.

KUTOKUKUTEGEMEA 
Mwanamke ambaye ana kusudio la kukuacha huanza kwa kuuondoa utegemezi. Ikiwa alikuwa anakuomba nauli, fedha ya matumizi, ada na huduma nyingine atasitisha bila kukuambia na bado utaona anaendelea kujimudu kama kawaida au kuteseka kimya kimya. Kuacha kukutegemea kama zamani ni dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri uwezekano wa kukuacha wakati wowote.

 " JITAMBUE MAKOSA YAKO ILI USIMKOSE"

MAAMBUKIZI YA KIFUA KIKUU(TB) YAZIDI NCHINI

Dar. Maambukizi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) yameendelea kushika kasi nchini ambapo Tanzania inatajwa kuwa ni nchi ya 22 duniani kwa kuwa na wagonjwa wengi wa TB huku ikishika nafasi ya sita kwa kuwa na wagonjwa wengi wa TB barani Afrika. 

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashidi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando alisema takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa mwaka 2013 wagonjwa wa Kifua Kikuu 65,000 waligunduliwa. 


Alizitaja aina mbili za Kifua kikuu ikiwamo cha mapafu ambacho hushambulia mapafu pekee na cha nje ya mapafu, huku akibainisha kuwa cha mapafu ndiyo kinaongoza hapa nchini. 


Alisema kwa mujibu wa takwimu za kawaida zinazopatikana kutoka katika vituo vya kutolewa huduma za afya , zinaonyesha kuwa maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa rika la vijana wenye umri kati ya miaka 25 na 44, kama ilivyo Virusi Vya Ukimwi. 


“Kifua Kikuu ni tatizo na kinashambulia zaidi vijana ambao ndiyo tegemeo la taifa hili, hivyo kudhoofisha uchumi wa nchi, hivyo wizara ili kunusuru kizazi hicho inaongeza juhudi za kuhakikisha inatokomeza kama siyo kukimaliza kabisa, alisema Mmbando. 


Alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), kati ya watu milioni tisa wanaougua ugonjwa huo duniani kwa mwaka, theluthi moja ya hao hawatambuliki katika mifumo ya sekta ya afya, huku sehemu ya hao milioni tatu wanaishi katika nchi masikini ikiwamo Tanzania. 


Alisema kwa Tanzania watu wanaoshambuliwa zaidi na ugonjwa huo ni katika makundi maalumu kama vile watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, watoto, wazee, wafungwa na watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama saratani na kisukari. 


Meneja Mipango wa Wizara hiyo Dk. Beatrice Mutayoba alisema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa kudhibiti ugonjwa huo bado ni tatizo kwa jamii na kila mwaka wagonjwa wapatao 63, 000 hugundulika. Huku Mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Morogoro, Mara, Arusha na Tanga ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi. 


“Hadi sasa kuna changamoto wa kuwabaini wagonjwa wa kifua kikuu, kwani kati ya wagonjwa 65,732 waliobainika katika takwimu za Kitaifa za kubaini wagonjwa zilizofanyika mwaka 2012, sawa na asilimia 54 pekee huku wagonjwa 56,000 hukosa kugundulika na kupata matibabu hivyo kuendelea kuwaambukiza wengine, ”alisema Dk. Mutayoba. 


Dk Mutayoba pia aliwataka wananchi kutodharau kifua cha aina yoyote kwa sababu hakuna kifua cha kawaida, hivyo kila anayekohoa anahitaji kupata ushauri wa daktari na vipimo. 


“Kifua siyo ugonjwa wa kurithi, kinaambukizwa, kina tiba na kinapona kabisa, hivyo kila anayekohoa anahitaji kupata tiba na vipimo sahihi badala ya kuona ni cha kawaida, ”alisema Mutayoba.

BAADA YA KUTUA ACT,AFANDE SELE ATANGAZA NIA

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, Suleimani Msindi ‘Afande sele’, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa Morogoro mjini kupitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania).


Msanii huyo ametangaza azma yake hiyo jana mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


“Niliumizwa baada ya kusikia kuwa eti katiba ya chama inasema kuwa mwanachama anayekwenda mahakamani kudai haki yake anakuwa amejivua uanachama wake.


Kwa chama kama Chadema sikuamini kama kingekuwa na sheria kandamizi kama hiyo ya kuzuia wanachama wake kwenda mahakamani, ambacho ndicho chombo cha mwisho kwa mtu kudai haki,” alisema.


Akielezea sababu nyingine iliyomfanya kujitoa Chadema imechangiwa na kuondolewa kwa Zitto Kabwe, ambaye alichangia kumhamasisha kujiunga na chama hicho.


“Jambo jingine nililojiuliza ni kwamba kama mti mbichi (Zitto), umetendwa hivyo je, mimi mkavu itakuwaje nikaona bora nivue ukamanda nivae utaifa kwanza,” Alisema Afande Sele

Sunday, March 22, 2015

OMBI LANGU KWENU

   Ndugu wapendwa,wenye upendo katika blogs, nawaombeni support yenu katika kuoipokea blog yangu  ambayo ni mpya katika soko la wapenda blog.
  Blog inaitwa Mchaka2 News <inamaana Mchaka Mchaka News>. Blog hii ni kwaajili ya kuwapa wapendwa habari mbalimbali ambazo zinajitokeza ulimwenguni. Tapenda kukujuza kila habari mpya inapotokea.
  Kwa upendo,umoja na ushirikiano nawaomba,kuperuzi na kunijuza mapungufu mbalimbali ya habari zitakazo kua zimewekwa na Mchaka2 News. 
  Kwa moyo wa dhati kabisa nawakaribisha tujumuike pamoja katika Mchaka2 News