Mchaka Zaidi

Tuesday, March 27, 2018

Mtanzania aliyeshinda Ubingwa wa Dunia wa Boxing Australia ametua leo


Jumamosi ya March 24 2018 bondia mtanzania Bruno Tarimo aliingia ulingoni kucheza pambano lake la 25 nchini Australia dhidi ya bondia kutoka Australia na kufanikiwa kumpiga na kushinda mkanda wa dunia wa WBA.
 Tarimo amewasili leo March 26 kutokea Australia aliposhinda Ubingwa wa dunia uzito wa kati KG 58 kwa kumshinda kwa point mpinzani wake Bilal Bid katika pambano lenye round 10 na kufanikiwa kutunza rekodi yake ya kucheza mapambani 25.
Bruno Tarimo katika mapambano 25 kashinda mapambano 23, akipoteza pambano moja na kutoka sare pambano moja, AyoTV imempata Bruno katika exclusive interview baada ya kuwasili Dar es Salaam akiwa na Mkanda wake wa Ubingwa wa Dunia WBA.

SOURCE: millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.