Kocha wa Manchester United Jose Mourinho alimsajili Luka Modric kutokea Tottehan Hotspurs kwenda Real Madrid mwaka 2012
katika kipindi cha usajili cha majira ya joto na kiungo huyo kukutana na wakati mgumu katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu Hispania LaLiga.
Hata hivyo mtandao wa express.co.uk umeripoti kuwa inawezekana Luka Modricasiendelee kuichezea tena Real Madrid na kuamua kurudi England kuungana na kocha wake wa zamani wa Real Madrid Jose Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha Man United.
Pamoja na kuwa mtandao wa Don Balon wa Hispania umeripoti na kuipa nafasi Man United ya kumsajili Modric mwisho wa msimu, vilabu vya Liverpool na Arsenalvinahusishwa kuhitaji saini ya Luka Modric pia.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.