Mchaka Zaidi

Wednesday, March 28, 2018

VIDEO: Argentina imechukua kipigo cha 6-1 dhidi ya Hispania ikimkosa Messi


Baada ya timu ya taifa ya Argentina kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Italia na kupata ushindi wa 2-0 weekend katika uwanja wa Etihad jijini Manchester huku staa wao Lionel Messi akiwa benchi, leo wamecheza game yao ya pili ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Hispania katika jiji la Madrid nchini Hispania.
Argentina leo wamemkosa staa wao Lionel Messi kutokana na kusumbuliwa na misuli na wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 6-1, magoli ya Hispania yamefungwa na Diego Costa dakika ya 12, Isco aliyefunga hat-trick dakika ya 27, 52 na 75, Thiagodakika ya 55 na Iago Aspas dakika ya 73 wakati goli la kufutia machozi la Argentinalikifungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 39.
Hat-trick ya Isco ndio inakuwa hat-trick yake ya kwanza akiichezea timu ya taifa ya Hispania ya wakubwa lakini jeraha la Lionel Messi limeanza kuleta presha kwa mashabiki wa timu yake ya FC Barcelona na kuanza kuhofia kama atapatikana katika mchezo dhidi ya Sevilla lakini wakiiwazia pia game yao ya robo fainali ya UEFA dhidi ya Roma itakayochezwa wiki ijayo Lionel Messi atakuwa fiti?

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.