Mchaka Zaidi

Sunday, April 17, 2016

VIDEO: Barabara za juu kuanza kutumika Dar, Rais Magufuli Kauzindua mradi wake jana



April 16 2016 Rais John Pombe Magufuli amefanya uzinduzi wa mradi wa barabara ya juu ‘Flyover’ Dar es salaam, barabara inayotarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2018.
Lengo likiwa ni kupunguza kero za usafiri katika jijila Dar es salaam, Barabara ambayo inatengenezwa chini ya usimamizi wa Serikali ya Japani, Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amesema ‘Kuna watu wakati tukibuni hili jambo walianza kuleta maneno na kusema ni jambo lisilowezekana, na sasa kazi imeanza na itawezekana, nataka tuifanye Tanzania kama Ulaya
Imefika wakati shughuli nyingi zinaharibika kwa sababu ya foleni, hata baadhi ya ndoa sasa zinavunjika kwa sababu watu wanachelewa kurudi majumbani kwao, sasa kwa huu mradi wa barabara za juu nahakika utatatua matatizo yote
Niwakumbushetu ndugu zangu, uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa kuwatumikia watanzania, tuweke uchama na usiasa pembeni na tusimame kwa pamoja maendeleo ya watanzania
Pia Rais Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika harakati zake za kuhakikisha Dar es salaam inakuwa safi ‘Nimpongeze sana mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa project yake aliyoianzisha katika kuifanya Dar es salaam kuwa safi, niwaombeni tumuunge mkono

Source:millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.